Psalms 149

Wimbo Wa Kumsifu Mungu Kwa Wema Wake

1 aMsifuni Bwana.

Mwimbieni Bwana wimbo mpya,
sifa zake katika kusanyiko la watakatifu.

2 bIsraeli na washangilie katika Muumba wao,
watu wa Sayuni na wafurahi katika Mfalme wao.
3 cNa walisifu jina lake kwa kucheza
na wampigie muziki kwa matari na kinubi.
4 dKwa maana Bwana anapendezwa na watu wake,
anawavika wanyenyekevu taji ya wokovu.
5 eWatakatifu washangilie katika heshima hii,
na waimbe kwa shangwe vitandani mwao.

6 fSifa za Mungu na ziwe vinywani mwao
na upanga ukatao kuwili mikononi mwao,
7 gili walipize mataifa kisasi
na adhabu juu ya mataifa,
8 hwawafunge wafalme wao kwa minyororo,
wakuu wao kwa pingu za chuma,
9 iili kuwafanyia hukumu iliyoandikwa dhidi yao.
Huu ndio utukufu wa watakatifu wake wote.

Msifuni Bwana.
Copyright information for SwhNEN